Kikosi cha polisi maalumu Jumamosi kilijiunga katika zoezi la kumsaka mtu ambaye hajafahamika aliye shambulia kundi kubwa la watu katika tamasha katika mji wa magharibi mwa Ujerumani, Solingen, na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine wanane, watano wakiwa katika hali mbaya.
Polisi imesema kwamba kwa sasa wanafanya msako mkubwa na mashuhuda na walio athirika wanafanyiwa mahojiano.
Polisi hawakuonyesha kama wamemtambua mtu huyo, bali waliwaonya watu kuwa makini hata kama watu wameanza kutoa salamu za pole kwa waathirika katika eneo la tukio.
Pia imeanzisha ukurasa rasmi ambao mashuhuda wanaweza kuweka picha za video, na taarifa nyingine zozote muhimu kuhusu shambulizi hilo.
Watu walitoa taarifa baada ya majira ya saa tatu na nusu usiku wa Ijumaa kuhusu uwepo wa mtu anaye shambuliwa watu.