Polisi wa Kenya Jumapili wamepiga marufuku wa wapinzani kufanya maandamano kutokana na kupanda kwa gharama za maisha wakisema maombi ya kufanyika maandamano hayo yalichelewa.
Licha ya tangazo hilo waandaaji wanasema wataendelea na tukio hilo.
Raila Odinga kiongozi wa chama cha Azimio la Umoja, aliitisha maandamano kesho katika mji mkuu wa Nairobi kutokana na mfumuko wa bei ambao mwezi Febuari ulifikia asilimia 9.2 katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Bwana Odinga pia anadai katika uchaguzi wa mwaka jana aliibiwa kura na kutangaza kutoitambua serekali ya rais William Ruto kuwa halali. Mkuu wa polisi wa Nairobi, Adamson Bungei, Jumapili amesema kwamba polisi walipokea maombi ya kufanya matukio mawili ya maandamano Jumamosi jioni, na mapema leo wakati utaratibu ni kutoa taarifa siku tatu kabla.