Polisi Kenya wakabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali

Mabomu ya machozi yakirushwa wakati wa mkutano ulioitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye anadai kuwa uchaguzi uliopita wa urais wa Kenya uliibiwa na analaumu serikali kwa kupanda kwa gharama za maisha jijini Nairobi, Machi 27, 2023.

Polisi nchini Kenya walikabiliana na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu, Nairobi, katika duru mpya ya maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani.

Polisi nchini Kenya walikabiliana na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu, Nairobi, katika duru mpya ya maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani.

Waandamanaji waliojitokeza mapema Jumanne asubuhi kuweka vizuizi kwenye barabara kuu kuzunguka jiji hilo waliwarushia mawe polisi, ambao walijibu kwa Mabomu ya kutoa machozi. Basi moja lilichomwa.

Biashara ilizorota katika Kaunti ya Kisumu, ngome ya upinzani, huku polisi wakikabiliana na waandamanaji.

Upinzani unataka kuchukuliwa hatua ili kukabiliana na gharama ya maisha na mageuzi kwa tume ya uchaguzi iliyosimamia uchaguzi wa mwaka jana ambao alishinda Rais William Ruto.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipingana na msimamo wa serikali kwamba maandamano hayo ya Jumanne si halali na kuwataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi.

Odinga alisema maandamano hayo yatakuwa ya amani. Mkuu huyo wa polisi alikuwa amepiga marufuku maandamano hayo, akitaja maandamano ya ghasia ya hapo awali yaliyopelekea biashara kadhaa kuporwa na raia wa Kenya kuibiwa.