Poland imeadhimisha miaka 85 tangu kuzuka kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati wa sherehe za maadhimisho ya kila mwaka yaliyofanyika alfajiri kukumbuka mashambulizi ya kwanza ya Nazi ya Ujerumani yaliyosababisha mgogoro huo hatari.
Karibu watu milioni sita walikufa katika mzozo huo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 50 kwa jumla, wakiwemo Wayahudi milioni sita waliofariki katika mauaji ya Holocaust, nusu yao wakiwa ni raia wa Poland.
Sherehe ya kumbukumbu ya leo Jumapili ilifanyika kitamaduni huko Westerplatte, kwenye pwani ya Baltic ya Poland, ambapo meli ya kivita ya Nazi ya Ujerumani ilifyatua risasi kwenye ngome ya Poland miaka 85 iliyopita hivi leo.
Akizungumza huko Westerplatte, Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk alisema somo katika Vita vya Pili vya Dunia “sio vya kufikirika” na lilifanana na vita katika nchi jirani ya Ukraine.