Mwanariadha mashuhuri kwenye mbio za walemavu za Olimpiki kutoka Afrika Kusini, Oscar Pistorius, leo Jumatano amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kutokana na mauwaji ya mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp yaliofanyika miaka mitatu iliopita.
Jaji Thokozile Masipa amepunguza hukumu hiyo kutoka miaka 15 kutokana na muda ambao Pistorius amekuwa kizuizini na pia kutokana na ulemavu wake.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Pistorius aliambia Mahakama kuwa alimpiga risasi Steenkamp kwa makosa akidhani kuwa ni mtu aliekuwa amevamia nyumba yake.
Steenkamp alipigwa risasi mara nne akiwa nyuma ya mlango wa choo usiku wa siku maarufu ya wapendanao ya Valentines mwaka wa 2013.
Waongoza mashitaka wamedai kuwa Pistorius alimuuwa Steenkamp kwa makusudi.