Pentagon kutuma wanajeshi kwenye mpaka wa kusini na Mexico

  • VOA News

Uzio kwenye mpaka wa kusini kati ya Marekani na Mexico.

Pentagon itaanza kupeleka hadi wanajeshi 1,500 ili kusaidia kulinda mpaka wa kusini na Mexico katika siku za karibuni.

White House imethibitisha hilo Jumatano na kwa hivyo kuanza mipango ya Rais Donald Trump aliyotia saini za amri ya kiutendaji muda mfupi baada ya kuapishwa, kulekea kushugulikia tatizo la uhamiaji.

Kaimu waziri wa Ulinzi, Robert Salesses alikuwa atie saini amri hiyo Jumatano ingawa haijabainika ni vikosi vipi vya jeshi vitapelekwa. Idadi yao pia huenda ikabadilika, na itabaki kuonekana iwapo wataishia kufanya kazi ya kudumisha sheria ambayo itaacha wanajeshi wa Marekani wakitekeleza majukumu tofauti kabisa ndani ya miongo mingi.

“Hili ni jambo ambalo rais Trump aliahidi kwenye kampeni zake,” amesema Karoline Leavit, msemaji wa White House. “Wamarekani wamekuwa wakisubiri wakati kama huu kwa wizara yetu ya Ulinzi kuhakikisha usalama wa ndani wa kina. Hicho ni kipaumbele kwa watu wa Marekani,” aliongeza.

Wanajeshi hao watajiunga na takriban walinzi wa Kitaifa 2,500 pamoja na vikosi vya ziada ambavyo tayari vipo kwenye mpaka huo. Kwa sasa hivi hakuna wanajeshi wowote waliyopo kwenye mpaka huo wa takriban urefu wa maili 2,000.