Ametoa wito kuhusiana na mjadala mkubwa unaoendelea ulaya kuhusu jinsi ya kudhibiti wahamiaji akiisishi jumuiya ya kimataifa kutafuta njia bora kudhibiti wingi wa wahamiaji katika bahari ya Mediterranean.
Amesema, “ninatoa wito wangu wa ndani kuhusu wahamiaji, wakimbizi na wengine wenye uhitaji wa ulinzi nchini Libya, sitakaa niwasahau, nasikia kilio chenu, na ninawaombea.”
Licha ya kwamba baba mtakatifu ametoa wito huo wa mabadiliko katika sera za wahamiaji na kueleza hisia za moyo wake katika maelezo yake kwa umma kwenye uwanja wa St Peters, mamia ya wahamiaji walikuwa katika bahari katikatika mwa Mediterranean wakisubiri kuokolewa kwa mujibu wa maafisa wa usalama.
Katika taarifa tofauti kundi la madaktari wasio na mipaka limesema wahamiaji 296 wamepanda meli yao ya Geo Barents ikisubiri kibali cha kuondoka Malta.
Wahamiaji sita wamepimwa na kukutwa na virusi vya corona, lakini kutokana na wingi wa watu ndani ya meli, ilikuwa ni vigumu kuwatenganisha na wengine.