Papa Francis kukosa misa ya mkesha wa mwaka mpya 2021

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis hataongoza misa ya kusherehekea mwaka mpya kwa sababu za kiafya.

Vatican imesema kwamba Papa Francis anahisi maumivu makali kwenye mguu wake wa kulia.

Hii ni mara ya kwanza kwa Papa Francis, mwenye umri wa miaka 84 kukosa kuhudhuria misa ya kufungua mwaka mpya, kwa sababu za kiafya.

Misa ya kukamilisha mwaka 2020 itaongozwa na Kadinali Giovanni Battista Re, na misa ya kukaribisha mwaka mpya 2021, itakayofanyika ijumaa, itaongozwa na Kadinali Pietro Parolin.

Vatican imesema kwamba Papa Francis ataingoza misa ya ijumaa adhuhuri.

Papa Francis ana matatizo ya kupata maumivu kutoka mgongoni hadi kwa sehemu ya chini ya mwili.

Wakati mwingine, huonekana akitembea kwa ugumu sana kutokana na maumivu.