Papa Francis, anayesumbuliwa na matatizo ya mapafu, alionekana akiwa ameketi katika kanisa lililopo kwenye makazi yake badala ya katika uwanja wa St. Peter's Square huku msaidizi akisoma ujumbe wa papa wa Jumapili.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 86, akiwa amevalia mavazi yake meupe ya kawaida na bandeji kwenye mkono wake wa kulia, alikuwa ameketi karibu na msaidizi wake wakati wa usomaji huo.
"Wapendwa kaka na dada. Jumapili njema. Leo, siwezi kutokea dirishani kwa sababu nina tatizo hili la kwenye mapafu,” Francis alisema.
Francis alikwenda hospitali ya Roma siku ya Jumamosi kwa uchunguzi ambao Vatikani ilisema ulifuta wasi wasi kuwa ana matatizo katika mapafu baada ya flu kumlazimisha kuakhirisha shughuli zake.