Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis, leo ametangaza marekebisho kwenye kanuni za jinai za kanisa hilo, ikiwemo adhabu dhidi ya mapadri na wengine wanaotumia nguvu, vitisho au kutumia vibaya madaraka kwa kujihusisha katika vitendo vya ngono.
Mapadri wanaotenda makosa hayo dhidi ya watoto na watu wazima wanaweza kutenguliwa, nao watumishi wa kawaida watafukuzwa kazi au walipe faini.
Marekebisho hayo yanaeleza kwamba maaskofu na viongozi wengine wa kidini wanaweza kuwajibishwa iwapo watashindwa kufanya uchunguzi kamili n kuwaadhibu mapadri wanaofanya vitendo viovu.
Kipengele kipya kinaeleza ni kitendo cha uhalifu kwa mapadri kumuhusisha mtoto kwenye utendaji wa ngono.