Baada ya sala yake ya kila wiki ya Malaika wa Mungu katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa amesema misaada ya kibinadamu lazima iruhusiwe kuingia kwa wingi nchini Myanmar na kusema watu lazima waheshimiwe katika eneo la Mashariki ya Kati linalokumbwa na vita kati ya Israel na Hamas.
Ametaja pia mateso ya watu nchini Ukraine.
Jeshi la Myanmar, ambalo liliiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa mwaka 2021, limekuwa likipambana na muungano wa majeshi wa makabila ya walio wachache yakipigana ili kumaliza udhibiti wa jeshi katika maeneo yao tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Francis amesema pia alipata taarifa “kwa furaha” kwamba kundi la watu wakiwemo watawa sita, waliachiliwa huru huko Haiti baada ya kushikiliwa mateka kwa karibu wiki nzima.
Wiki iliyopita alikuwa ameomba waachiliwe.