Papa Francis siku ya Jumatano alisema "amehuzunishwa sana" na shambulizi la risasi katika shule moja huko Texas na kuua takriban watoto 19 na walimu wawili, na kutaka kuwepo na udhibiti mkubwa wa silaha.
Watu waliofurika katika uwanja wa St. Peter's kwa kusikiliza hotuba yake ya kila wiki walipongeza hotuba yake, iliyotoa siku moja baada ya shambulizi baya zaidi la risasi shuleni nchini Marekani katika karibu muongo mmoja.
“Nimeumizwa sana na mauaji haya katika shule ya msingi
huko Texas. Ninawaombea watoto na watu wazima waliouawa
na kwa familia zao," Francis alisema juu ya shambulizi la risasi huko Uvalde, Texas.