Papa Francis anasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 85

Papa Francis akipita karibu na mti wa Krismasi wakati wa hadhara kuu kwenye Ukumbi wa Paul VI ulioko Vatican Desemba 01, 2021. (Picha na Filippo MONTEFORTE / AFP)

Baba mtakatifu Fransis anasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa leo ambapo anatimiza miaka 85. mrithi wake alistaafu akiwa na umri kama huu na baba mtakatifu wa mwisho kuishi Maisha marefu zaidi alikuwa LEO XIII zaidi ya karne iliyopita.

Baba mtakatifu Francis anasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa Ijumaa ambapo anatimiza miaka 85. mrithi wake alistaafu akiwa na umri kama huu na baba mtakatifu wa mwisho kuishi Maisha marefu zaidi alikuwa LEO XIII zaidi ya karne iliyopita.

Taarifa zinasema licha ya Baba Mtakatifu kufanyiwa tiba ya upasuaji wa utumbo katika kipindi cha majira ya joto anaendelea vyema na kufanya kazi zake. hadi sasa katika miaka yake nane ya upapa aliyotumikia , Francis amejihusisha na kufanya mabadiliko ndani ya kanisa waziwazi hata wakati wa shutuma za unyanyasaji wa kingono zilizowakabili baadhi ya maafisa na watumishi katika kanisa, amelifanya kanisa katoliki ndani na nje ya Vatican kuhudumia zaidi watu wa kawaida.

Katika kipindi cha janga la Corona amepata ukosoaji mkubwa kwa sababu ya juhudi zake za kuifanya dunia kujiimarisha katika masuala ya mazingira na uchumi.

Katika vita dhidi ya rushwa Baba Mtakatifu alifanya maamuzi ya kuweka masharti ya afisa wa kanisa kupokea zawadi ya sio zaidi ya dola 45. alipitisha sheria ya kuruhusu makadinari na maaskofu kuhukumiwa kwa uhalifu na mahakama ya vativan wakikutwa na makosa .