Papa Francis ametakiwa kukomesha manyanyaso kanisani

Papa Francis akihutubia wanafunzi katika chuo kukii cha kikatoliki cha Louvain, Ottignies-Louvain-la-Neuve, Ubelgium, Sept. 28, 2024

Papa Francis amekamilisha ziara yake nchini Ubelgiji leo Jumapili, ambapo aliangazia sana ukosoaji dhidi ya kanisa katoliki kutokana na shutuma za unyanyasaji.

Papa, mwenye umri wa miaka 87, ameshinkizwa na viongozi wa ngazi ya juu katika hafla 5 tofauti wakati wa ziara yake ya siku tatu, kuchukua hatua dhidi ya unyanyasaji ndani ya kanisa hilo.

Katika kikao na maafisa wa ngazi ya juu wa Ubelgiji, mfalme Philippe na waziri mkuu Alexander De Croo, wametaka kuchukuliwa madhubuti kuwasaidia waathiriwa wa manyanyaso yaliyotekelezwa na makuhani wa kanisa katoliki.

Katika hafla nyingine, maafisa katika vyuo vikuu viwili vya katolini wamepinga msimamo wa Papa Francis kuhusu majukumu ya wanawake kanisani na katika jamii.

Japo hakuzungumzia ukosoaji aliokumbana nao wakti wa misa katika uwanha wa michezo wa mfalme Baudouin, Papa Francis amekosoa vikali manyanyaso yanayofanywa na makuhani kanisani.