Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mtu maarufu kuliko wote katika Kanisa Katoliki, ambaye amekuwa akishutumiwa kuhusika na kitendo cha kuwaharibu watoto wa kiume na wa chuo cha seminari McCarrick ni kadinali wa kwanza kupoteza wadhifa wake katika kumbukumbu ya miaka ya hivi karibuni.
Kashfa inayomkabili imelishtua Kanisa la American Church kwa sababu alikuwa kiongozi mwenye kuheshimika kwa miongo mingi na alikuwa karibu na papa wengine na marais.
“Papa amekubali kujiuzulu kwake kutoka katika bodi ya makadinali na ameagiza kuwa asimamishwe kuhubiri, na kulazimishwa kukaa nyumbani katika nyumba itakayopangwa awepo, akiishi maisha ya kufanya ibada na kutubia mpaka pale tuhuma hizo dhidi yake zitakapo fanyiwa uchunguzi rasmi," tamko lililotolewa na Vatican limeeleza.
Mwezi uliopita, maafisa wa Kanisa la American Church wamesema kuwa madai kuwa kadinali huyo alimharibu kijana miaka takriban 50 iliyopita ni ya kweli.
Tangu wakati huo, watu kadhaa wamejitokeza wakidai kuwa McCarrick aliwalizimisha kufanya mapenzi nao katika nyumba iliyoko ufukweni mwa bahari huko New Jersey wakati wakiwa wanafunzi wa chuo cha kidini wakijifunza upadri.
McCarrick anasema yeye “hakumbuki chochote” kati ya tuhuma za kumharibu kijana miaka 50 iliyopita lakini hakutoa maoni yoyote juu ya madai hayo ya kuwaharibu vijana na mtoto mdogo madai yaliyoletwa dhidi yake.