Wawakilishi wa jeshi na kikosi cha wanamgambo, ambao wamekuwa wakipigana kwa karibu mwezi mmoja, walisaini makubaliano mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa “tamko la nia ya dhati kuwalinda raia wa Sudan,” alisema afisa wa Marekani anayeshiriki katika mazungumzo hayo.
Makubaliano hayo yanazitaka pande zote mbili kwa ujumla kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia nchini, kuruhusu kurejeshwa kwa umeme, maji na huduma za msingi, kuwaondoa maafisa wa usalama katika hospitali na kupanga “mazishi ya heshima” ya waliouawa katika mapigano.
Mazungumzo bado yanaendelea ili kufikia makubaliano mapya ya muda ya kuruhusu misaada, huku kukiwa pendekezo mezani la kusitisha mapigano kwa siku 10, afisa huyo wa Marekani ambaye aliomba jina lajke lihifadhiwe alisema.