Asemavyo Leodger Tenga
Wachambuzi wa soka wanasema mechi ya fainali kati ya Senegal na Algeria itakuwa ngumu sana kwa sababu Algeria na ubavu wake wote tangu mwaka 1990 inataka kulichukua kombe hili tena ikiwa ni mara ya pili endapo wataishinda Senegal.
Na kwa upande wa timu ya taifa ya Senegal nayo inataka kuandika historia ya kunyakua kombe la AFCON mwaka 2019, na kuwekwa kwenye rekodi kama taifa bingwa barani Afrika japo watamkosa mchezaji wao muhimu kiungo wa kati Kalidou Koulibaly ambaye alipewa kadi mbili za njano katika mechi zilizopita ndani ya michuano hii.
Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) imemnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF Leodger Tenga kwenye mazungumzo aliyofanya na Mwanahabri wetu Sunday Shomari jijini Cairo – akisema “ Koulibaly ni mchezaji mzuri hata ukimuona uchezaji wake …. kwa hiyo mimi ningefurahi kumuona, kwa sababu nataka wachezaji wazuri kabisa duniani wawepo kwenye fainali”.
Mshindi wa tatu
Kwa upande wa mchezaji John Obi Mikel mechi hiyo ndio itakuwa ya mwisho, ambapo ataagwa kiuchezaji, kwani ndio anastaafu kuchezea timu yake ya taifa ya Nigeria.
Mechi ya fainali
Kiwanja cha soka cha kimataifa cha Cairo ndani ya wiki hii kinahodhi mechi ya mwisho ya michuano ya AFCON 2019 ambayo ni mchezo wa fainali kati ya Senegal na Algeria ijumaa tarehe 19 Julai.
Mpaka muda huu vyombo vya usalama vimeshajipanga kiulinzi zaidi na mashabiki wa pande zote mbili nao wako tayari kufurika uwanjani.
Maandalizi
Hii ni ishara ya kuwepo maandalizi ya mchezo huo dimbani kama ilivyokuwa katika siku ya ufunguzi wa michuano hii ya AFCON 2019 tarehe 21 June au shamra shamra zake zikawa zaidi kuliko siku hiyo ya ufunguzi kutokana na kishindo cha fainali.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Cairo, Misri