Waziri huyo ameiambia VOA katika mahojiano maalum wiki hii kwamba anadhani kanuni na masharti ambayo tayari yalikuwepo na China ya wazalishaji wa kujitegemea wa umeme yana mashaka na yanapaswa kupitiwa upya.
Miradi ya kufua umeme ambayo ilitengenezwa katika muongo uliopita, ulisaidia kumaliza kipindi kirefu ya kukosekana kwa umeme.
Hata hivyo mikataba inataka Pakistan, kulipia kiwango chote cha uzalishaji cha uwezo wa kinu cha kufua umeme bila kuzingatia kiwango cha umeme kinachotakiwa kutumika.
Kutokana na kushindwa kufanikisha ukuwaji wa sekta ya viwanda kwa Pakistan kuilifanya taifa hilo kulipia kiwango ambacho hakitumiki kilicho tarajiwa kutumiwa na viwanda zaidi.
Hali hiyo kumeifanya nchi hiyo kuwa na bili kubwa ya kulipia uzalishaji wa umeme.