Pakistan italipa zaidi ya dola milioni 2 kwa familia za wafanyakazi wa China waliouawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga mwaka huu.
Wafanyakazi watano wa China na dereva wao wa Pakistani waliuawa Machi 26 wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipovamia gari lililokuwa na vilipuzi kwenye msafara wao katika jimbo la kaskazini magharibi la Khyber Pakhtunkhwa.
Kamati ya uratibu wa uchumi, chombo kikuu cha uchumi cha Pakistan kiliidhinisha fedha dola milioni 2.58 Alhamisi kama fidia kwa familia za waathirika wa kigeni.
ECC, inayoongozwa na Waziri wa Fedha wa Pakistani Muhammad Aurangzeb, pia imeidhinisha karibu dola 9,000 za fidia kwa familia ya raia wa Pakistani aliyeuawa.