Paetongtarn Shinawatra ndie Waziri Mkuu mpya wa Thailand

Waziri vMkuu mpya wa Thailand, Paetongtarn Shinawatra

Wabunge walimuidhinisha Paetongtarn wa chama cha Pheu Thai kama Waziri Mkuu kwa kura 319 dhidi ya 145.

Binti wa bilionea Thaksin Shinawatra mwenye miaka 37 amekuwa waziri mkuu wa Thailand leo Ijumaa, mwanafamilia wa tatu wa ukoo wenye ushawishi mkubwa kisiasa lakini wenye mgawanyiko katika kuiongoza nchi hiyo.

Paetongtarn Shinawatra, kiongozi mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Thailand kama mfalme wa kikatiba, na mwanamke wa pili baada ya shangazi yake Yingluck, anachukua madaraka baada ya maamuzi mawili ya mahakama ambayo yalitupilia mbali siasa za ufalme huo zinazoingiza machafuko.

Atajitahidi kuepuka hatima ya baba yake na shangazi yake, ambao wote waliondolewa kama Waziri Mkuu na jeshi wakati wa mapambano ya miongo miwili ya madaraka kati ya Thaksin na utawala wa ki-Conservative katika jeshi, unaounga mkono utawala wa kifalme.

Wabunge walimuidhinisha Paetongtarn wa chama cha Pheu Thai kama waziri mkuu kwa kura 319 dhidi ya 145, Spika wa Baraza la Wawakilishi alitangaza moja kwa moja kwa televisheni.