Hafla hiyo iliyodhaminiwa na Hollywood Foreign Press Association na kuongozwa na mchekeshaji maarufu, Seth Myers, ilihudhuriwa na nyota wengi katika fanui ya uigizaji, ikiwa ni pamoja na msanii maarufu na wa muda mrefu, Oprah Winfrey.
Winfrey alipata tuzo la Cecil B Demille, la msanii aliyechangia pakubwa uigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni kwenye maisha yake.
Msanii huyo aliyefahamika mno kwa sababu ya filamu iitwayo 'Color Purple,' aliweka rekodi kwa kuwa mwanamke mweusi wa kwanza kupata tuzo hiyo.
Huku akionekana karibu kububujikwa na machozi, Oprah alieleza jinsi katika safari yake ya usanii, amekuwa akisumbuka akilini kwa sababu ya taarifa kuhusu udhlilishaji wa kingono dhidi ya wanawake katika fani mbalimbali.
Hotuba yake ya kusisimua iliangazia suala la kudhlilishwa kingono kwa wasanii baada ya wanawake kadhaa wa Hollywood kujitokeza mwaka uliopita na kudai kwamba walidhalilishwa kwa njia moja au nyingine.
Waliohudhuri hafla hiyo walivaa nguo nyeusi kama ishara ya kuwaunga mkono wanawake ambao wamejitokeza na kusema kwama walidhalilishwa kingono.
Filamu iitwayo ‘Three Billboards outside Ebbing, Missouri,’ ilipata tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na filamu bora Zaidi kwa uigizaji yani Drama.
Katika fani ya vichekesho, filamu iitwayo ‘Lady bird,’ ilishinda.
Mwelekezi bora Zaidi wa filamu katika mwaka wa 2017 ni Guillermo Dol Toro, aliyeelekeza filamu, ‘The shape of water.’
Kwa upande wa filamu za lugha za kigeni, filamu ‘In the Fade,’ iliyotumia lugha za kifaransa na Kijerumani, ilinyakua ushindi.
Kwa upande wa waigizaji bora, mchezaji katika vipindi vya televisheni, Sterling Brown, ambaye ni Mmarekani mweusi, alitoa hotuba ya kusisimua alipopata tuzo la mchezaji bora.
Brown alimsifu mzalishaji wa filamu, ‘This is US,’ kwa kumpa nafasi katika sinema hiyo akiwa mtu mweusi wa pekee.
Mcheza filamu maarufu, Nicole Kidman, pia alituza, kwa nafasi aliyoicheza kwenye filamu, ‘Big Little lies.’
Lakini labda kilele cha tamasha hizo kilikuwa hotuba yake msanii maarufu Oprah Winfrey.