Ongezeko la bei ya umeme lazidisha ukali wa maisha Zimbabwe

Kutokana na gharama za umeme kuongezeka na wananchi kutoweza kupata umeme au kushindwa kulipia mtoto wa miaka 9 akisoma kwa kutumia mshumaa, Harare, Zimbabwe, Julai 23, 2019.

Bei ya umeme ilipanda kwa asilimia 320 nchini Zimbabwe Jumatano ikiwa ni ongezeko la mara ya pili ndani ya miezi mitatu.

Kupanda kwa bei ya umeme kumesababisha hali ya maisha kuwa mbaya zaidi katika nchi hiyo iliyo na mzozo mbaya kuliko wowote wa uchumi uliowahi kutokea nchini humo.

Ongezeko hilo kubwa la bei ya umeme linaacha wengine kutumia mishumaa.

Baadhi ya wafanyabiashara wanalalamika kwamba kutokana na umeme kuwa hautabiriki hawawezi kufikisha huduma na bidhaa kwa wateja wao.

Maafisa wanasema ongezeko hilo lilihitajika ili shirika la umeme nchini humo liweze kufanya kazi yake na kudumisha vifaa vyake na kununua mafuta ya majenereta.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.