Nyota wa zamani OJ Simpson aachiwa huru Marekani

O J Simpson

Nyota wa zamani na msanii maarufu nchini Marekani O J Simpson amepata msamaha baada ya kukaa gerezani kwa miaka tisa, huko jimbo la Nevada nchini Marekani.

Alihukumiwa kutumikia kifungo baada ya kukutikana na makosa ya wizi wa kutumia nguvu na silaha na pia alikabiliwa na mashtaka mengine 10 ya mwaka 2017 yaliomhusisha na tukio moja huko Vegas.

Mnamo mwaka 1995 mashtaka ya kumuua aliyekuwa mke wake Nocole Brown Simpson na rafiki wake Ron Goodman yaliondolewa.

Picha za kwenye mitandao zilimuonyesha akisaini stakabadhi na akiondoka kituo cha Lovelock Correctional Center mapema Jumapili.

Mwaka 2008, miaka 13 baada ya kufutiwa mashitaka ya 'Kesi ya karne' alipatikana na hatia ya uvamizi wa hotel.

Yeye pamoja na kundi la watu wengine watano walivamia Hoteli na kuelekea katika eneo linalotunza vifaa vya michezo, wakachukua vitu ambavyo alidai vilikuwa vyake kutokana na ushiriki wake michezoni.

Katika harakati za msamaha huu, OJ Simpson aliwaambia maafisa wa jopo la kutoa msamaha kuwa vitu alivyochukua hata hivyo vilikuja kugundulika kuwa vilikuwa vyake.

"Nimeishi maisha yasiyo ya mgogoro" alisema katika kikao kilichodumu kwa saa moja.