Ofisi ya rais Afrika Kusini yapokea vyema tangazo la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu- ICC

Rais na kiongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia bungeni Mei 1, 2024. Picha na RODGER BOSCH / AFP.

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema Jumatatu imepokea vyema tangazo la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema Jumatatu imepokea vyema tangazo la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ikisema iliomba hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mkuu wake wa ulinzi na viongozi watatu wa Hamas kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Sheria lazima itumike kwa usawa kwa wote ili kuzingatia utawala wa sheria za kimataifa, kuhakikisha uwajibikaji kwa wale wanaofanya uhalifu wa kutisha na kulinda haki za waathirika, ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa ilisema katika taarifa yake.

Afŕika Kusini, ambayo ndio sauti inayoongoza katika kupigania haki za Wapalestina, pia imepeleka kesi dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikiishutumu kwa mauaji ya halaiki, ambayo Israel inakanusha.

Viongozi wa Israel na Hamas wamekanusha madai ya kufanya uhalifu wa kivita, na wawakilishi wa pande zote mbili wamekosoa uamuzi wa mwendesha mashtaka.