Obasanjo afanya ibada ya ukumbusho kwa heshima ya Jimmy Carter

  • VOA Swahili

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo. Picha ya maktaba.

Rais wa zamani wa Nigeria Chifu Olusegun Obasanjo amefanya ibada ya ukumbusho huko Abeokuta kusini magharibi mwa Nigeria kwa heshima ya Rais zamani wa Marekani Jimmy Carter ambaye alifariki  decemba 29 na kuzikwa wiki iliyopita.

Akiongea kwa sauti yenye huzuni kuhusu kiongozi huyu wa zamani wa Marekania ambaye amesema kuwa ni rafiki yake wa binafsi, Obasanjo alisema atamkosa sana lakini anamini kuwa wataonanatena tena peponi.

“Nita mkosa sana lakini ninajua tukutana tena peponi,”alisema.

Obasanjo alimtaja marehemu Carter kuwa mtu mwadilifu aliyejitolea kwa nguvu zake zote katika harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa utawala wa kibeberu na ubaguzi wa rangi kusuni mwa Afrika.

Akizungumzia ukaribu wao kama marafiki na viongozi wenye ajenda moja ya kuona kuheshimiwa kwa haki za binadamu na usawa wa watu wote kote ulimwenguni, Abasanjo alisema kuwa Jimmy Carter ndiye sababu yake kuwa hai hivi leo.

“Yeye ndiye sababu ya mimi kuwa hai leo”.

Obasanjo alisema Nigeria na Afrika na haswa jumuiya ya kimataifa imepoteza rafiki na mshiriki aliyefanya kazi kwa bidii na kwa ridhaa kwa ajili ya amani ya kimataifa.

Jimmy Carter alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Nigeria akitokea Brazil, March 31, 1978, na kupokelewa mjini Lagos na Obasanjo, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa kijeshi la Nigeria.

Ziara hiyo ilikuwa ya maana sana kwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha vita vya Nigeria dhidi ya utawala wa kibaguzi Afrika Kusini, Angola, Namibia, Zimbabwe na Msumbiji ambapo Nigeria iliwekeza rasilimali nyingi .