Nimefanya makubwa hata kuliko wanaumme - Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba amefaya kazi vizuri sana kama rais wa nchi hiyo, kuliko wanaumme walio mtagulia ofisini.

Rais huyo wa Tanzania amesema kwamba alikabiliwa na changamoto kubwa ya watu kutoamini kwamba anaweza kuongoza taifa hilo kwa sababu ni mwanamke. Amesema kwamba kwa sasa ameshinda chagamoto hizo.

Samia alikuwa akizugumza katika hafla ya kiuchumi mjii Accra Ghana, ikiwa ni ziara yake ya kwanza Afrika magharibi tangu alipoigia madarakani kufuatia kifo cha John Pombe Magufuli.

“Ilikuwa vigumu sana kwa watu nchini Tanzania kuniamini. Hawakuwa na Imani kwamba ninaweza kuongoza taifa jinsi wanaume walivyokuwa wakifanya. Hiyo ndiyo ilikuwa changamoto kubwa,” amesema wakati wa mkutano wa kila mwaka wa benki ya maendeleo Afrika (AfDB)

“Mwaka huu, nimeonyesha nguvu za mwanamke. Nimeongoza nchi namna walivyofanya wanaume na wakati mwingine, kuwashinda hao wanaume,” ameongeza kusema Samia.

Samia ndiye rais mwanamke mwenye mamlaka mengi Afrika kwa sasa. Rais wa Ethiopia hana mamlaka kwani nguvu nyingi zipo katika ofisi ya Waziri mkuu.

Mkutano huo wa Ghana ulihudhuriwa na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na Azali Assoumani wa Comoros.