Nigeria yazindua mpango wa N-Power kuwaptia vijana ajira

Serikali ya Nigeria imezindua mradi mkubwa wa uandikishaji ajira kupitia mtandao ili kutowa mafunzo nafasi za ajira kwa vijana. Mradi huo umepokelewa kwa hamu kubwa na wakati huo huo kuibuwa mvutano kidogo kutoka kwa watu wanaojaribu kuingia kwenye ukurasa huo mtaandaoni.

Serikali iliafungua ukurasa wa uandikishaji kwa kutumia mtandao N-Power mwezi huu na kusema kuwa itaandika takriban wahitimu wa chuo kikuu nusu millioni kufanya kazi katika sekta mbalimbali, hususan afya, elimu na kilimo. Ukurasa huo wa tovoti unatangaza kutoa mafunzo ya ajira kwa watu ambao si wahitimu katika maeneo kama technologia .

Lakini vijana wanaotafuta ajira wanasema kuna tatizo. Mtandao ulikuwa unazimika mara kwa mara.

Mohammed anasema, amekuwa akikabiliwa na ugumu kidogo. Kwa zaidi ya siku 3 sasa kila nnapojaribu kuingia kwenye ukurasa huo nakabiliwa na tatizo. Kwa hiyo nadhani huwenda hata huo ukurasa hauko sawa.

Huyo ni Usman Mohammed mwenye umri wa miaka 25. Ana shahada ya uzamili katika udhibiti wa mazingira na inaonekana kuwa anayo anwani sahihi ya ukurasa wa N-Power.gov.ng. Anarejea tena kwenye mtandao.

Mohammed anasema, tatizo liko palepale. Labda nadhani nikijaribu tena leo huwenda nikawa miongozi wa watu walobahatika kuingia kwenye ukurasa huo.

Mara nyengine, ukibonyeza unapata ujumbe wa kuwepo hitilafu. Mara nyengine hupati ujumbe wowote.

Ukurasa unakushauri ujaribu tena baada ya dakika chache. Huo ndio ushauri timu ya N-Power inatowa kupitia mtandao wa Twitter. Lakini takriban asli mia 42 ya watu walojaribu kujaza fomu wiki ilopita wanasema hawakuweza kufanya hivyo.

Idara ya taifa ya takwimu inasema taktiban theluthi tano ya ya wanigeria walio chini ya umri wa miaka 34 hawana ajira.

Msongomano huo mkubwa katika ukurasa wa mtandaoni wa N-Power, unashiria kiu kwa nafasi za ajira kwa taifa lenye watu wengi zaidi duniani, lakini baadhi wana matumaini.

Bulus Mungopark anaishi katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri.

Bulus anasema, nina shaka kwa sababu miaka yote hii, hakuna kitu kilichoonyesha kuwa Nigeria iko tayari kuajiri vijana.

Serikali inasema takriban wanigeria laki 4 walijiandikisha kwenye N-Power katika masaa 36 ya kwanza, na ukurasa huo umetazamwa zaidi mara millioni 35.

Mipango ya awali ya serikali ya kuajiri yalipelekea mkanyangano .

Hapo mwaka 2014 watu 7 waliuwawa pale maelfu ya wanigeria walipomiminika uwanja wa kitaifa wa michezo mjini Abuja kujiandikisha kupata ajira katika idara ya uhamiaji. Hapo mwaka 2008 mpango mwengine wa kuajriri uliplekea watu 12 kufariki.