Sarafu ya Nigeria yashuka thamani

Nigerian naira notes are seen in this picture illustration March 15, 2016.

Kwa miezi kadhaa, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amekua akipinga wazo la kushusha dhamani ya sarafu ya nchi yake - naira. Msimamo huo ulibadilika jumatatu baada ya Benki kuu kuchukua hatua ya kuweka sarafu hiyo kwenye soko huru na kusababisha mara moja thamani ya Naira kushuka kwa asilimia 30 dhidi ya dola ya marekani. Lakini huwenda hatua hiyo imeokoa kudorora kwa uchumi wa Nigeria unaotegemea mafuta. Wachumi wamesema kuiweka Naira kuwa imara kulimaliza akiba ya fedha za kigeni ya Nigeria na kuwatia hofu wawekezaji. Mashambulizi ya wanamgambo dhidi ya miundo mbinu nyeti ya mafuta pamoja na kushuka kwa bei za mafuta na upungufu wa sarafu za kigeni kumehujumu uchumi mkubwa wa barani Afrika na hivyo kushushwa thamani ya sarafu ya Nigeria ni jambo lisiloweza kuepushwa.