Nigeria:Watu 12 wauawa katika mashambulizi tofauti

Ramani wa Nigeria

Watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa au kutekwa nyara katika msururu wa mashambulizi kaskazini mashariki na katikati mwa Nigeria, polisi na maafisa walisema Jumatatu.

Ukosefu wa usalama ni changamoto kubwa katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika wakati rais mpya anaratajiwa kuapishwa mwezi ujao kufuatia uchaguzi uliopingwa na upinzani.

Watu wenye silaha wasiojulikana Jumatatu walivamia kijiji cha Dabna katika wilaya ya Hong katika jimbo la kaskazini mashariki la Adamawa na kuua watu watatu, msemaji wa polisi wa eneo hilo Suleiman Nguroje amesema, akiongeza kuwa nyumba zilichomwa moto.

Hakuna kundi lililodai kuhusika licha ya kuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram hufanya mashambulizi ya hapa na pale katika eneo la karibu na msitu wa Sambisa katika jimbo jirani la Borno.

Jumatatu pia, watu wenye silaha walishambulia jamii katika kijiji cha Oganenigu katika wilaya ya Dekina katika jimbo la katikati la Kogi, kulingana na maafisa wa eneo hilo.

Msemaji wa gavana Muhammed Onogwu amesema mwanasiasa wa eneo hilo aliuawa huku wengine wakiathiriwa na shambulio hilo baya.