Nigeria imetia saini mkataba wa biashara huru Afrika kwenye mkutano wa AU

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari akitia saini mkataba wa biashara huru Afrika kwenye mkutano wa AU mjini Niamey, Niger

Viongozi wa Afrika walikutana Jumapili kuzindua eneo la biashara huru kwa bara hilo ambapo kama inafanikiwa itawaunganisha watu bilioni 1.3 ili kubuni ushirika wa kiuchumi wa dola trilioni 3.4 na kuongoza katika maendeleo ya enzi mpya

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametia saini mkataba wa biashara huru Afrika wa hadi dola trilioni tatu, alithibitisha msemaji wake kwa shirika la habari la Reuters. Ikiwa na uchumi mkubwa sana barani Afrika uamuzi wa Nigeria kutia saini mkataba huo ilikuwa kuonesha njia ya kuongeza matumaini ya mbeleni. Ilikuwa moja ya nchi za mwisho mwisho kujizatiti katika mkataba huo.

Viongozi katika bara la Afrika walikutana Jumapili kuzindua eneo la biashara huru kwa bara hilo ambapo kama inafanikiwa itawaunganisha watu bilioni 1.3 ili kubuni ushirika wa kiuchumi wa dola trilioni 3.4 na kuongoza katika maendeleo ya enzi mpya.

Baada ya miaka minne ya mazungumzo makubaliano ya kuunda ushirika wa biashara wa nchi 55 uliafikiwa mwezi Machi na kutoa njia kwenye mkutano uliofanyika Jumapili wa Umoja wa Afrika-AU nchini Niger mahala ambapo washiriki watazindua nchi ipi itakuwa mwenyeji wa makao makuu ya biashara ya eneo wakati biashara itakapoanza na kuzungumzia namna ambavyo biashara hiyo itafanya kazi.