.Netanyahu asisitiza kuendeleza mashambulizi

Ukuta wa makazi ya watu uliotobolewa na shambulizi la roketi kutoka ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Jumapili hakupanga mwisho wowote wa haraka wa kumalizika mashambulizi mabaya ya anga Jumapili huko Gaza, saa kadhaa baada ya ndege zake za kijeshi za kivita kupiga na kuyaangusha majengo matatu na kuua watu wasiopungua 42.

Katika tangazo la TV aliiambia serikali ya Kiyahudi kwamba mashambulizi yalikuwa yakiendelea kwa nguvu zote na yatachukua muda.

Natumai haitachukua muda mrefu, Netanyahu alikiambia kipindi cha TV cha Face the Nation cha CBS nchini Marekani. Lakini alisema mwisho wa mashambulizi hayo haukuwa wa haraka licha ya juhudi za kimataifa za kusuluhisha mzozo huo wakati mashambulizi ya pande zote ya makombora kati ya vikosi vya Israeli na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza yakiendelea.

Tulishambuliwa na Hamas, mashambulizi yasiyokuwa na sababu yoyote dhidi ya Jerusalem, mji mkuu wa Israeli, Netanyahu alisema.

Wakati huo huo mhariri mkuu wa shirka la habari la Associated Press anataka uchunguzi huru juu ya shambulio la anga la Israeli ambalo lililenga na kuharibu jengo Gaza City ambalo lililokuwa na ofisi za AP, Al-Jazeera na vyombo vingine vya habari.

Mhariri mtendaji wa AP, Sally Buzbee, anasema serikali ya Israeli bado haijatoa ushahidi wa wazi kuunga mkono shambulio lake, ambalo liliangusha jengo la ghorofa 12 la al-Jalaa.

Jeshi la Israeli limesema kwamba Hamas ilitumia jengo hilo kwa ofisi ya ujasusi wa kijeshi na utengenezaji wa silaha, na msemaji anasema Israeli inakusanya ushahidi kuwapa Marekani. Taasisi ya Waandishi Wasio na Mipaka inaitaka mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ichunguze bomu hilo kama uhalifu wa kivita.