Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameandika kwenye mtandao wa kijamii Ijumaa kwamba kutambuliwa kwa taifa la Palestina kutatoa faida kubwa kwa ugaidi ambao haujawahi kutokea.
Ametoa maoni yake baada ya kuzungumza na Rais wa Marekani, Joe Biden, na baraza la mawaziri la Israel, pamoja na ripoti ya gazeti la Washington Post, kwamba Marekani na washirika wake wa Kiarabu wanapanga kuendeleza azimio la mataifa mawili kwa mzozo unaoendelea wa Mashariki ya Kati.
Netanyahu ameandika katika mtandao wa X, zamani Twitter kwamba Israel, inakataa moja kwa moja maagizo ya kimataifa kuhusu mipango ya kudumu na Wapalestina.
Ameandika kwamba mipango yoyote na Wapalestina itafikiwa tu kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande zote bila ya masharti.