Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jumatatu kwamba ilikuwa ajali mbaya sana ambapo shambulio lililowalenga wanamgambo wa Hamas katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah liliwaua Wapalestina 45 waliokuwa wakipata hifadhi katika kambi ya wakimbizi na kuwajeruhi wengine 200.
Licha ya juhudi zetu nzuri, sio kuwadhuru wale ambao hawakuhusika, kwa bahati mbaya kosa la kusikitisha lilitokea usiku wa Jumatatu. Tunachunguza kesi hiyo, Netanyahu aliliambia bunge la Israel. Wanamgambo wawili wa ngazi ya juu wa Hamas waliuawa katika shambulio hilo.
Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amelaani tukio hilo akisema katika taarifa yake, “Picha kutoka kambi hiyo ni za kutisha na zinaonyesha hakuna mabadiliko ya wazi katika mbinu na njia za vita zinazotumiwa na Israel ambazo tayari zimesababisha vifo vingi vya raia”.