Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela hatahudhuria sherehe za miaka 100 ya ANC. Maafisa wa ANC wameelezea matumaini kuwa kiongozi huyo aliyepambana dhidi ya ubaguzi mwenye umri wa miaka 93 atahudhuria sherehe hizo.
Katibu mkuu wa chama Gwede Mantashe alitangaza Ijumaa kwamba Mandela ataikosa shughuli hiyo akisema yupo kwenye hali nzuri lakini ni mzee sana.
Bw. Mandela na chama cha ANC waliongoza mapambano dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa weupe wachache . Mwaka 1994 alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini na chama hicho kimeongoza nchi tangu wakati huo.
Sherehe zimeanza Ijumaa na tukio kuu limepangwa kufanyika jumapili , ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 ya chama cha ANC.