Ndege ya Pakistan ya biashara yaondoka Kabul

Your browser doesn’t support HTML5

Safari za ndege ya abiria zaanza kati ya Pakistan na Afghanistan

Ndege ya kimataifa ya biashara imeondoka Kabul Jumatatu ikiwa ya kwanza tangu Taliban kuchukua madaraka mwezi uliopita ikitoa ishara ya matumaini kwa Waafghanistan ambao bado wanataabika kuondoka nchini kwao.

Jumatatu asubuhi ndege ya shirika la ndege la Pakistan ilitua Kabul kabla ya kugeuza kwenda Islamabad.

Takriban watu 709 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakielekea mji mkuu wa Pakistan wengi wao wakiwa raia wa Afghanistan ambao ni ndugu wa wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa kama vile World Bank, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege.

Mataifa mengi yaliyoko kwenye umoja wa NATO yamekubali muda umewaishia kuondoa maelfu ya watu walioko katika hali ya hatari nchini Afghanistan kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa kwa makubaliano ya Marekani na Taliban. Hata hivyo shirika la ndege la Qatar ilifanya operesheni ya ndege kadhaa za abiria nje ya Kabul wiki iliyopita ikiwa imebeba zaidi abiria wa kigeni na Waafghanistan waliokosa ndege wakati wa kuondolewa.

shirika la ndege la Afghanistan limeanza safari zake za ndani septemba 3.