Ndege isiyo na rubani yashambulia msafara Syria

Picha ya maktaba

Ndege zisizo na rubani zimeshambulia msafara wa malori mashariki mwa Syria, Jumapili usiku muda mfupi baada ya kuvuka mpaka kutokea Iraq.

Wanaharakati wa upinzani wa Syria, na redio inayounga mkono serekali zimethibitisha tukio hilo lakini hakuna taarifa za haraka kama kuna vifo vimetokea.

Shambulizi hilo limetokea wakatia mvutano ukiwa umeongezeka baina ya Iran na wapinzani wake wa kikanda.

Hakuna taarifa za uhakika za anayehusika na shambulizi hilo dhidi ya msafara katika mpaka wa Syria wa eneo la Boukamal, ambapo ni ngome ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

Kundi la uangalizi wa haki za binadamu Syria lenye makazi yake Uingereza limesema ndege isiyo na rubani inaonekana kuwa imetoka kwa muungano unaoongozwa na Marekani, likiongeza kwamba ililenga malori sita yenye majokofu.