Nchi nane zenye nguvu duniani G 8 zimetoa wito wa kujiuzulu kwa kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi huku wakiahidi karibu dola elfu 40 za msaada kwa mataifa ya kiarabu ambayo yanajaribu kuimarisha demokrasia.
Taarifa hiyo imekuja katika azimio la mwisho la pamoja wakati wa kukamilisha mkutano wa siku mbili uliohusisha nchi nane zenye nguvu duniani huko Deauville, Ufaransa.
Mizozo ya mataifa ya kiarabu ya mashariki ya kati na kaskazini mwa afrika ndiyo yaliyokuwa katika ajenda ya juu kwenye mkutano huo.
Azimio hilo la mwisho lenye nguvu limesema ‘ Gadhafi hana nafasi huru, katika demokrasia ya Libya. lazima aondoke”. Pia imetoa mwito wa sitisho la haraka la matumizi ya nguvu dhidi ya raia yanayofanywa na vikosi vya usalama vya Libya na kusema kuwa wahusika lazima wawajibishwe.
Wito wa kutaka Gadhafi kujiuzulu ulitolewa na nchi nane zenye nguvu duniani katika mkutano wao huko Ufaransa.