Nchi zote mbili ziliwasilisha maombi ya kujiunga na NATO mwezi Mei mwaka huu, kinyume na misimamo ya muda mrefu, ya kutofungamana na upande wowote katika kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
"Hii ni siku nzuri kwa Finland na Sweden, na siku nzuri kwa NATO,” amesema Katibu Mkuu wa NATO, Jen Stoltenberg.
“Kwa kuwa mataifa 32 yametia saini itifaki hizi, tutakuwa na nguvu zaidi na watu wetu watakuwa salama zaidi tunapokabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa," Stoltenberg aliongeza.
Aliendelea kusema kuwa mlango wa NATO bado uko wazi kwa “demokrasia za Ulaya ambazo ziko tayari kuchangia usalama wetu wa pamoja."
Baada ya itifaki za kujiunga kutiwa saini, kila moja ya nchi wanachama wa NATO, sasa zinapaswa kuziidhinisha azma hiyo ya Finland na Sweden, kulingana na taratibu zao za kitaifa.
Licha ya makubalino katika umoja huo, pingamizi la awali ya mjumbe Uturuki linaweza kusababisha matatizo kwa ajili ya kukamilisha uanachama.
Wiki iliyopita rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdowan alionya kwamba Ankara inaweza kuendelea kuzuia utaratibu huo, kama nchi hizo mbili zitashindwa kufikia matakwa ya uturuki kuwarejesha washukiwa wa ugaidi wenye uhusiano na makundi haramu ya kikurdi au mtandao wa kiongozi wa kidini aliyoko uhamishoni anayeshutumiwa kwa mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 2016 huko uturuki.