Mwimbaji Natalie Cole afariki dunia

Natalie Cole

Mwimbaji maarufu wa nchini Marekani Natalie Cole amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda. Alikuwa na umri wa miaka 65.

Taarifa kutoka kwa familia yake inasema mwimbaji huyo alifariki Alhamisi usiku saa chache kabla mwaka mpya kuingia mjini Los Angeles. Natalie Cole alikuwa mtoto wa mwimbaji maarufu sana Marekani katika miaka ya 50 na 60 Nat King Cole.

Your browser doesn’t support HTML5

Wimbo - Unforgettable

Moja ya wimbo wake uliompatia sifa sana ulikuwa "Unforgettable" ambao aliweza kuunganisha sauti yake na baba yake ingawa tayari alikuwa amekufa na kutoa kibao hicho.

Natalie Cole amewahi kushinda tuzo kadha za Grammy kwa wimbo kama vile "This Will Be" na vile vile "Unforgettable."

Familia yake imetoa taarifa ikisema kuwa alikuwa na matatizo kadha ya afya katika miaka ya karibuni na alipambana kiasi alichoweza hadi kifo chake Alhamisi usiku.