NASA yaahirisha safari ya anga za juu

  • VOA News
Shirika la anga za juu la Marekani, NASA limechelewesha safari ijayo ya anga ili kutoa muda zaidi katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kushugulikia chombo cha Boeing kinachosafirisha wanaanga chenye matatizo.

Shirika hilo Jumanne limesema kwamba linasogeza mbele safari ya chombo cha SpaceX kinachochukuwa wanaanga wanne kutoka mwezi huu hadi ujao.

Kwa sasa inatarajia kufanya safari hiyo Septemba 24 ikiwa ni tarehe ya mapema zaidi.

Maafisa wamesema kufanya hivyo kutawapa muda zaidi wa kuchunguza matatizo ya nguvu na uvujaji ambayo yalikumba chombo cha Boeing Starliner baada ya safari yake ya kwanza ya Juni, kikuwa na wanaanga ndani yake.

Jumanne kilifikisha kipindi cha miezi miwili kikiwa kimekwamba katika kituo cha anga za juu na marubani wake wa majaribio Butch Wilmore na Sunita Williams, waliopaswa kurejea duniani katikati ya Juni.