Nancy Reagan azikwa

wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza la Nancy wakati wa mazishi

Nancy Reagan atakumbukwa kama mwanamke imara na machachari pia, lakini mtu ambaye kwa asilimia 100 alitoa muda wake kwa mume wake rais Ronald Reagan.

Mke wa rais wa zamani wa marekani Nancy Reagan amekumbukwa kwa kicheko na machozi Ijumaa na waombolezaji 1,000 walioalikwa katika mazishi yake kwenye maktaba ya Rais Ronald Reagan huko Semi valley , Carlifonia.

Nancy Reagan amefariki akiwa na umri wa miaka 94 kutokana na shinikizo la damu kwenye moyo Jumapili iliyopita huko Bel Air katika jimbo la Carlifonia.

Mke wa rais wa sasa Michelle Obama aliwakilisha ikulu ya Marakeni katika mazishi hayo Ijumaa. Rais Barack Obama katika hotuba yake ya wiki alisema yeye kama rais , “anajua ni jinsi gani inavyomaanisha kuwa na mwenzi wako aliye imara na rais Reagan alibahatika , kama yeye.”

Orodha ndefu ya marafiki wa familia ya Reagan wakiwemo wa consevativu wa Republicans na waliberali wa DemocratS walihudhuria mazishi hayo. Walikuwemo familia ya ikulu kuanzia miaka 60 iliyopita , Caroline Kennedy, Steven Ford, rais wa zamani George W Bush , mke wa rais wa zamani Hillary Clinton, Laura Bush na Rosalynn Carter.

Kwa upande wa Hollywood walikuwemo waigizaji Tom Selleck na Bo Derek, waimbaji Johnny Mathis na Wayne Newton.

Nancy Reagan atakumbukwa kama mwanamke imara na machachari pia, lakini mtu ambaye kwa asilimia 100 alitoa muda wake kwa mume wake rais Ronald Reagan.

Wakati rais Ronald Reagan alipopata matatizo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu – Alzheimer’s, Nancy Reagan alikuwa mshauri mkubwa katika utafiti ambao madaktari waliamini kuwa ungewezeza kupelekea kupata tiba ya ugonjwa huo.

Rais Barack Obama aliamuru bendera zote za Marekani katika majengo ya Serikali kupepelea nusu mlingoti hadi Ijumaa usiku wakati Nancy Reagan alipokuwa anazikwa pembeni ya kaburi la mume wake kwenye makataka ya Rais iliyopewa jina lake.