Simba jijini Nairobi.

Askari wa KWS akilenga Simba alietoroka kutoka mbuga ya wanyama ya Nairobi.

Mji wa Nairobi katika siku za hivi karibuni umeshuhudia visa vya wanayama pori kutoka kwenye mbuga ya kitaifa ya Nairobi.

Mji wa Nairobi katika siku za hivi karibuni umeshuhudia visa vya wanayama pori kutoka kwenye mbuga ya kitaifa ya Nairobi. Miongoni mwa wanyama hao yule ambae ametia hofu zaidi ni Simba ambae kwa hakika ni myama hatari kwa binadamu. Harrison Kamau amaefutilia matukio hayo kwa kina akianza na historia ya mbuga hiyo maarufu duniani.

Your browser doesn’t support HTML5

Simba Nairobi

Mbuga ya kitaifa ya Nairobi ilipata jina hilo kutokana na kupakana na mji wa Nairobi. Mbuga hiyo ilioanzishwa mwaka wa 1946 iko umbali wa takriban kilomita 7 kusini mwa jiji hilo ikikalia kwenye ekari 29,000 za ardhi kwenye sehemu ya milima na eneo lijulikanalo kama Athi Kapiti. Ndani ya mbuga hiyo ya kilomita 45 mraba, kuna wanyama aina tofauti miongoni mwao Simba, Vifaru,Fisi,Twiga,Chui na ndege wa aina tofauti. Sikiliza masimulizi zaidi.