Wakati wa hotuba yake ya kwanza mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa,Bennett hakutaja mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina, na badala yake alionekana kulaumu Iran kama adui mkubwa kwenye usalama wa kimataifa.“Program ya nyuklia ya Iran imefika kilele, nao ustahimilivu wetu pia umefika mwisho,” Ameongeza Bennett.
Baada ya kufanyika kwa uchaguzi usiokamilika kwa miaka miwili, Bennett hatimaye alichukua nafasi ya waziri mkuu wa muda mrefu Benjamin Netanyahu mwezi Juni baada ya kuunda serikali ya muungano wa vyama tofauti vya kisiasa, suala ambalo llilibadili siasa za Israel
Bennett aliongeza kusema kwamba ni dhahiri kwa kila mwenye macho kwamba nia ya Iran ni kuchukua udhibiti wa kieneo kwa kutumia uwezo wake wa ki nyuklia. Kiongozi huyo amemtaja rais mpya wa Iran Ebrahim Rais kama mchinjaji wa Tehran kutokana na jukumu lake la awali la kukanadamiza wakosoaji pamoja na kutoa ufadhili kwa maadui wa Israel.