Mwanasheria mkuu wa Marekani atakiwa kutoa maelezo mbele ya bunge.

Mwansheria mkuu wa Marekani William Barrr.

Barr alitoa muhtasari wa kurasa nne kuhusu ripoti ya Mueller kuhusiana na shutuma za kampeni ya Trump kushirikiana na Russia.

Mwenyekiti wa kamati ya sheria ya Bunge amemtaka mwanasheria mkuu William Barr kutoa maelezo ya mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller ambayo duru zinaeleza kwamba taarifa ya Mueller ilikuwa mbaya zaidi kwa rais Trump kuliko Bar alivyolieleza Bunge la Marekani.

Barr alitoa muhtasari wa kurasa nne Machi 24 kuhusu ripoti ya Mueller kuhusiana na shutuma za kampeni ya Trump kushirikiana na Russia ili kuvutia matokeo ya uchaguzi upande wake.

Barr amesema timu ya Mueller haikupata ushahidi wowote wa Trump kushirikiana na Russia au wafanyakazi katika kampeni zake kushirikiana au kufanya kazi na Russia.

Mwanasheria mkuu huyo pia alisema Mueller hakuhitimisha kama kama rais hakuingilia kati uchunguzi huo na kuongeza haikutajwa kama hana hatia. Barr alisema yeye na naibu wake Rod Rosenstein waliamua kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki rais na kuingilia kati haki.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.