Mwanasheria mkuu wa Israel amuonya Netanyahu kuingilia mfumo wa mahakama

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu.

Afisa mkuu wa sheria wa Israel, anamuonya Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, kujiepusha na shinikizo la baraza lake la mawaziri la kurekebisha mfumo wa mahakama.

Mpango huo ambao wakosoaji wanasema unaweza kuipa serikali madaraka yasiyo na kikomo.

Mwanasheria Mkuu wa Israel, Gali Baharav-Miara, alisema katika barua kwa Netanyahu iliyowekwa hadharani Alhamisi, kwamba lazima ajiepushe kama sehemu ya jukumu lake kama waziri mkuu kuhusika katika mipango inayohusiana na mfumo wa sheria.

Netanyahu amekuwa akikabiliwa na kesi ya rushwa inayohusisha madai ya ulaghai, uvunjaji wa uaminifu na kupokea hongo, ambayo yote ameyakanusha.

Mapendekezo ya marekebisho ya mfumo wa mahakama, yataruhusu idadi kubwa ya wabunge wa nchi hiyo yenye viti 120 kubatilisha maamuzi ya Mahakama.