Mwanamuziki maarufu Tina Turner afariki akiwa na umri wa miaka 83

Manamuziki Tina Turner

Tina Turner, mwimbaji maarufu mzaliwa wa Marekani ambaye aliacha jamii ya wakulima, kuwa katika mahusiano magumu na kuibuka kuwa mmoja wa wasanii bora zaidi, aliaga dunia Jumatano akiwa na umri wa miaka 83.

Mwakilishi wake alisema alifariki kwa amani baada ya kuugua kwa muda mrefu nyumbani kwake katika mjhi wa Küsnacht karibu na Zurich, Uswizi.

Turner alianza harakati zake za uimabaji katika miaka ya 1950 wakati muziki aina ya rock 'n' roll ulipoanza, na akaibuka kuwa mahiri katika tasmnia hiyo.

Katika video ya wimbo wake ulioongoza kwenye chati WA "What's Love Got to Do with It," ambapo aliyaita mapenzi "hisia zilizotumiwa," Turner alijitokeza kama mwanamitindo wa kuigwa katika miaka 1980, alipokuwa akipita katika mitaa ya Jiji la New York akiwa na nywele zake za kimanjano zilizokolea, amevaa koti la jean lililopunguzwa, minisketi na viatu vyenye visigino virefu , maarufu stiletto.

Wakati mwingine akipewa jina la utani la "Malkia wa Rock 'n' Roll," Turner alishinda Tuzo zake sita kati ya nane za Grammy, katika miaka ya 1980.

Mika ya 80 ilishuhudia nyimbo zake kadhaa zikiingia kwenye Top 40, zikiwemo "Typical Male," "The Best," "Private Dancer" na "Better Be Good To Me."

Tamasha lake la 1988 mjini Rio de Janeiro, Brazil, lilivutia watu 180,000, ambalo linasalia kuwa moja ya hadhira kubwa zaidi ya tamasha kwa msanii yeyote.

Alizaliwa Anna Mae Bullock tarehe 26 mwezi Novemba mwaka 1939, katika jamii ya vijijini ya Tennessee ya Nutbush, ambayo alielezea katika wimbo wake wa 1973 "Nutbush City Limits" kama "jamii ya zamani tulivu, na mji wa farasi mmoja."