Mwanaharakati wa demokrasia wa Hong Kong, alikamatwa Jumanne miezi michache baada ya kuachiliwa kutoka gerezani kwa kukiuka sheria kali ya usalama wa taifa katika eneo hilo.
Shirika la habari la Reuters, linasema Albert Ho, mwenye umri wa miaka 71 alifungwa pingu na kuondolewa nyumbani kwake kwa gari, kulingana na shahidi. Albert Ho, aliwahi kuongoza Muungano wa Hong Kong unaounga mkono demokrasia kabla ya kukamatwa mwaka 2021 na kushtakiwa kwa kuchochea uasi.
Alikaa jela kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuachiliwa Agosti mwaka jana kwa matibabu, kulingana na Reuters.
AFP inasema iligundua kutoka kwa chanzo kisichojulikana kwamba Ho alikamatwa na kushtakiwa kwa kuingilia kati mashahidi wakati akiwa nje kwa dhamana.