Mwanaharakati mashuhuri wa kupigania demokrasia kutoka Hong Kong ameshitakiwa mapema leo kwa kutoeleza serikali kuhusu mchango aliopokea kutoka kwa mfanyabiashara mmoja mashuhuri anaepinga China.
Leung Kwok Hung, ambae pia anajulikana kama "Long Hair," anatuhumiwa kwa kupokea dola 32,000 kutoka kwa Jimmy Lai ambae ni mmiliki wa gazeti la 'Apple' la kila siku.
Tume huru ya kupambana na ufisadi ya Hong Kong imemfungulia Leung, mwenye umri wa miaka 60, shitaka la matumizi mabaya ya ofisi ya umma hatia ambao Leung anaamini imechochewa na siasa.
Leong amekuwa kwenye baraza la Bunge la Hong Kong tangu 2004.
Hofu kuwa China huenda inaongeza juhudi za kushikilia Hong Kong hasa baada ya ufichuzi uliotolewa na muuza vitabu wa Hong Kong anaedaiwa kuzuiliwa China miezi 8 iliopita.