Dawit Isaak alikuwa miongoni wa kundi la takriban watu darzeni 2 wakiwemo mawaziri na wabunge pamoja na wanahabari, waliokamatwa kwenye msako wa Septemba 2001. Isaak sasa amepewa tuzo ya Edelstam kutokana na mchango wake wa kupigania haki za kujieleza, Imani na kulindwa kwa haki za binadamu, taasisi ya Edelstam imesema kupitia taarifa.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa Isaak ni mfungwa kwa kihisia wakati kundi la Wanahabari wasio na Mipaka, RSF, likisema kuwa Isaak pamoja na wenzake waliofungwa ndiyo wanahabari waliozuiliwa kwa muda mrefu zaidi ulimwenguni.
Wataalam wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishinikiza Asmara kumuachilia mara moja. Eritrea haijakuwa ikitoa taarifa kumhusu, na kuna hofu kwamba huenda hayupo hai tena, na iwapo yu hai basi ana umri wa miaka 60.