Tangu kuwa chukuwa watoto watatu wenye asili ya Kiafrika kuwalea, ameweza kupata mafunzo kuhusu mambo yasiyo rahisi ya maisha, na jinsi rangi inavyoathiri taswira ya tabia ya mwanafunzi au namna anavyoendelea na masomo.
Poole anasema binti yake Nyara akiiwa katika kidato cha kwanza “alikua anaadhibiwa kwa kutoka darasani wakati watoto walikuwa wakimchokoza kutokana na rangi yake.”
Nyara amepimwa akiwa na tatizo la kutoweza kuwa makini na matatizo ya kiwewesasa na kakake Carter aliyechukuliwa pia kulelewa.
Poole anasema mtaalamu wa sikolojia wa shule za umaa alipompima Carter alipokua chekechea na kueleza kuwa alikuwa na mwenedo wa kuwa na vurugu, hasira, na uharibifu.
Poole alisisitiza kwamba taabia hizo zifutwe kwenye mpango maalum wa masomo ya mototo wake, akihofia kwamba atatumbukia katika “mfumo wa shule hadi jela.. vipi unaweza kuorodhesha mambo kama haya ya vurugu – kwa mvulana mwenye umri wa miaka 6”, aliuliza.
Baadhi ya waatalkamu wanaamini kumchukua mtoto kumlea na kabila lake yote yanaweza kuathiri wanafunzi na jinsi wanavyochukuliwa.
\Nicolas Zell, mtafiti wa masuala ya sikolojia mjini Washington, pamoja na mwenzake walizingatia jinsi watoto wanaolelewa na watu wasio wazaazi wao wanavyoendelea shule, katika ripoti yaoya mwaka 2018.
[[https://ifstudies.org/blog/the-adoptive-difference-new-evidence-on-how-adopted-children-perform-in-school]].
Utafiti huo wao uligunduwa kwamba watoto walochukuliwa kulelewa mara nyingi wanamatatizo ya kusoma na tabia kuliko wanafunzi wengine, pengiune ikimulika ukosefu wa kuwa makini mwanzoni mwa utoto wao.
Amesaema, “ wattoto wanaolelewa wanamatatizo ya adabu darasani na wanamatatizo fulani kuendelea pamoja na watoto wengine kwa kiwango kikubwa kuliko watoto wenye wazazi wao.
Hata hivyo watoto walochukuliwa tangu wachanga kulelewa hawana matatizo hayo anasema Zell.
Bila ya kujali umroi Zell anasema baadhi ya watoto wanaolelewa wanakabiliwa na utata mwengine.
“kwa ujumbe watoto weusi huwa na kiwango fulani cha juu cha matatizo miongoni mwa watoto wanaolelewa na wale wanaoishi na waziazi wao.”
Kamamwalimu na mlezi, Poole anaona mfumo wa elimu wenyewe ni sababu ya baadhi ya changamoto za watoto hao.
“ukiangalia katika mtaala, kwa sehemu kubwa ni ya wazungu” anasisitiza. “Ukiangalia vitabu, vingi vyao ni ya wazungu. Na mambo haya yote byamewatenganisha watoto wa rangi nyingine.”
Hilo si jambo la ajabu kwa Constance Lindsay, naibu profesa wa elimu katika chuo kikuu cha North Carolina. Amesomea uhusiano kati ya walimu na wanafunzi.
Anasema, “ukiwa na mwalimu mzungu ambae hajafunzwa masuala ya utamatuni mbali mbali na vipi kufanya kazi na wanafunzi wa rangi mbali mbali , inaweza kua na madhara kwa wanafunzi.: Anaongezea kusema “kuwa na mwalimu wa rangi sawa kwa wanafunzi weusi kunapunguza kiiwango cha kuwaadhbu wanafunziu,” kama vile kusimamishwa au kufukuzwa.
Lindsay pia aliandika ripoti na mwenzake mwaka 2017
[[http://ftp.iza.org/dp10630.pdf]] iliyofuatilia jinsi wanafunzi katika shule za msingi na sekondari. Iligundua kwamba wale ambao angalau walikuwa na mwalimu mmoja mweusi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kwenda chuo kikuu na kuacha masomo akiwa shule ya sekondari.
Lindsay anaeleza hali hiyo kuwa ni ile ya mfano mzuri.
“ikiwa unakulia katika nyumba ambayoi hakuna mtu mweusi aliyehitimu chuo kikuu na unaweza kumona moja shuleni ambae ni mwalimu wako , hiyo huwenda ikawa ishara kwako wewe kwamba , mimi ninaweza kufanya hivyo pia!” Anasema Lindsay.
Bi. Poole anasema watoto wake wananawiri tangu walipohamishwa kutoka shule ya mtaa wao wa Seattle hadishule za umaa za kitongoji cha wilaya ya Highline ambako anasomesha na ambako anasema walimu wamepatiwa mafunzo ya kufahamu tofauti ya watu wa rangi mbali mbali na usawa.
Anakiri kwamba yeye pia anabidi kuhamasihwa.
“Na hata nikiwa mwalimu. Nina maana masomo niliyojifunza kama mama mzungu na kuwa na watoto weusi ni namna ubaguzi umeoteshwa mizizi katika umbo la shule zetu kwa kiwango kikubwa.” Anasema Poole “na sikufahamu haya yote kabla mnilipowapata watoto weusi.”